Siku ya leo October 24, 2019 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize amerejea kufanya mahojiano kwa mara ya kwanza toka alipoondoka WCB na Clouds FM kupitia kipindi cha XXL, Harmonize amesema kuwa aliimisi sana amani na alikuwa akitamani sana kukutana na watu wa Clouds na kushuhudia ngoma zake zikipigwa kama awali.
Pia Harmonize amedai kuwa kwa sasa hawako vizuri sana na uongozi wake uliopita wa WCB na kueleza sababu zilizopeleka kutokuwaalika kwenye harusi yake aliyoifunga miezi kadhaa iliyopita.
..>>>“Amani ndio kitu nilikimiss kipindi ngoma zangu hazipigwi Clouds, nilikuwa natamani kama hivi nikutane na na nyie tupige story! Naheshimu misingi ya kibiashara lakini now tuko good Mimi ni Harmonize lakini nyuma ya Harmonize kuna Rajabu, Kwenye mambo ya kibinadamu Rajabu lazima ahusike ndio maana nilishiriki kwenye mazishi ya Ruge, Nilichokifanya hakikuniletea matatizo kwenye uongozi wangu uliopita”
“Sitaki kusema uongo, Mahusiano yangu na uongozi wangu uliopita sio kama zamani, na kuhusu wao kushindwa kuhudhuria ndoa yangu mimi niliweka nadhiri kuwa siku ya ndoa yangu ningependa wahudhuriaji wawe ni ndugu zangu niloishi nao vizuri kijijini”
“Kuikweli kule sijaondoka kwa ubaya, tumefuata sheria na taratibu za mkataba! Nilitakiwa kulipa million 500 na baadhi ya gharama, kiukweli ckuwa na pesa lakini nimeuza baadhi ya mali zangu ili nifanikiwe kulipa hiyo pesa na kwa asilimia kubwa nimelipa bado asilimia chache tu ili niweze kutumia kitu chochote kinachomuhusu Harmonize”
“Kauli ya Rais ni sheria! Kwahiyo siwezi kuikataa, nahisi hata wananchi wa Tandahimba hawawezi kuikataa! Kwahiyo tutakaa chini mimi na wananchi wa Tandahimba tujue tunaifanyaje kauli ya Mh Rais”
“Jembe ni mtu aliyekuwa akinisupport tangu kitambo, Baada ya kuvunja mkataba na lebo yangu ya nyuma! Jembe akaamua kuanza kunisupport japo watu wengi wamekuwa wakimtafsiri vibaya na kuhisi kwamba yeye ndio chanzo cha kunifanya niondoke kule lakini sio kweli” – Harmonize