SIMU ZA INFIX NA TECNO KUPATA ANDROID 10 KABLA YA 2020




Kama wewe ni mmiliki wa simu ya TECNO au INFINIX basi
habari njema ikufikie kwani hivi karibuni kampun hizo zinategemea
kutoa mfumo mpya wa Android 10 kwa baadhi ya simu zake.

Kwa mujibu wa google transsion ambayo ni kampuni mama ya
kampuni za TECNO , INFINIX pamoja na ITEL imetangazwa kwenye
list ya kampuni za simu ambazo zinategemea kusasisha mfumo mpya wa
Android 10 kwenye simu zake kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kampuni
nyingine zilizotajwa kwenye list hiyo ni pamoja na ASUS, LG, MOTOROLA,
OPPO, REALME, SAMSUNG, SHARP, SONY na VIVO.

Hata hivyo kwa mujibu wa Ripoti kutoka XDA developer, Google imetangaza
kuwa kila simu ya Android ambayo inategemewa kuingia siokoni kuanzia mwaka
2020 ni lazima izinduliwe ikiwa na mfumo mpya wa Android 10 na sio vingine
Hii ni habari njema kwa watumiaji wa simu za TECNO pamoja na INFINIX
kwani kama unavyojua mara nyingi kampuni za TECNO pamoja na INFINIX
zimekuwa na utaratibu wa kuzindua simu mpya za Android zikiwa na mfumo
wa zamani wa Android bila kujali kuwa kunao mfumo mpya wa Android
kwa kipindi hicho


Mbali na hayo kampuni ya TECNO kwa sasa bado ipo kwenye majaribio ya
mfumo huo wa Android 10 kwenye simu zake za spark 3 pro, ambapo simu hiyo
inategemewa kuwa moja kati ya simu kutoka kampuni ya TECNO zitakazopata
mfumo huo mpya wa ANDROID 10



Mpaka sasa kampuni zote za TECNO na INFINIX bado hazijatangaza list kamili
ya simu ambazo zitapokea mfumo huo mpya wa ANDROID 10 kabla ya mwisho
wa mwaka huu 2019. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti mbali mbali simu zote za
TECNO SPARK 3 PRO, TECNO PHANTOM 9, TECNO CAMON 12, TECNO SPARK 4,
INFINIX HOT 8 na INFINIX S5   Zinategemewa kuwa kwenye list ya simu zitakazo
pata mfumo huo mpya




endelea kufatilia blog hii kwa mengi zaidi
Previous Post Next Post