Wachezaji wa Southampton waiacha mishahara ya baada ya kipigo 9-0



Kipigo cha magoli 9-0 kilichowapata Southampton  dhidi ya Leicester City kilichotokea weekend iliyopita kimewafanya wachezaji wa Southampton kukataa kupokea mishahara yao ya wiki hii kutokana na kipigo hicho cha historia.
Wachezaji wa Southampton wameamua kuwa mishahara yao ya Ijumaa waitoa msaada kwa taasisi ya Saints Foundation, wachezaji hao wamefikia maamuzi hayo kwa pamoja na benchi lao la ufundi.
Hata hivyo kipigo cha magoli 9-0 walichofungwa Sothampton kinakuwa ni miongoni mwa vipigo vitatu vikubwa vilivyowahi kutokea katika historia ya EPL (Baada ya 04/03/1995 Man United 9-0 Ipswich na 22/11/2009 Tottenham 9-1 Wigan)
Previous Post Next Post