Watu 20, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni iliyotolewa na Benki Kuu (BOT) kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi-Kasumulu,Wilaya ya Kyela.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Urich Matei, amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana katika oparesheni ya kushtukizwa na endelevu inayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini.